WALINZI WA UFALME

Kama tunavyofahamu kitabu cha Biblia sio kitabu cha kidini bali, Biblia inahusu mambo kumi ambayo ni Ufalme, mfalme, familia ya kifalme, serikali ya Ufalme, katiba ya Ufalme, uchumi wa Ufalme, sheria ya Ufalme, mila ya Ufalme, hati ya kisheria na jeshi la Ufalme.

Ndani ya Ufalme kuna majeshi, kuna nchi inaitwa mbinguni ipo hapa duniani ambayo sisi tuliookolewa tunaishi ndani yake. Yesu alisema mtu lazima azaliwe mara ya pili ndipo aingie kwenye Ufalme wa Mungu awe raia wa mbinguni. Jeshi hili la Ufalme linaitwa Malaika watakatifu. Malaika hawa ni watumishi wetu ambao wanatutumikia na kutulinda.

Kwenye agano jipya HHenoko ametajwa alikuwepo akaishi na kutwaliwa na Mungu, pia kwenye agano jipya tunaona kwamba Henoko alikuwepo lakini alitwaliwa na Mungu.

WAEBRANIA 11: 5 “kwa imani HHenoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.”

Yuda naye aliandika kwamba huyu Henoko aliandika kitabu.

YUDA1: 14 na HHenoko, mtu wa saba baada ya adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, angalia, bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

Tukiangalia kwenye uandikishwaji wa Biblia tunaona, Paulo alikuwa ulaya(urumi) akaandika barua kwa Wakorintho, akaandika nyingine kwa wagiriki nayo ikaenda Ugiriki, baadaye wazee wa imani wakaanza kuzikusanya pamoja wakaanza kuzipangilia lakini hazikuwa na mistari wala mpangilio kama huu wa sasahivi tulio na, vitabu hivyo vikiwa kwenye maeneo mbalimbali vilikusanywa pamoja vikaitwa Biblia maana yake Bibros’ (mkusanyiko wa vitabu). Mwaka 1948 mtu mmoja ambaye ni mchungaji wa mbuzi na Ngombe alikuwa akichunga mifugo yake lakini ghafla hakuona mbuzi wameelekea wapi kutoka mahali alipo ndipo akaamua kurusha jiwe kwenye moja ya mapango na mara akasikia jiwe moja linalia kama ngoma ndipo akaamua kuwaita watu wakaja kulivunja wakagundua kumbe ni jiwe la kutengenezwa wakakuta vitabu vyote vya kwenye Biblia na vitabu vingine ambavyo havipo kwenye Biblia. Wakati wanaangalia ndipo wakakuta na kitabu cha Henoko ambacho ndicho kitabu kinachoelezea ukubwa wa Malaika mmoja ana urefu wa mita 145 na unene mkubwa sana,

Biblia inasema miguu ya Malaika ni kama shaba iliyosuguliwa sana, amefungwa mshipi kifuani mwake, na macho yake ni kama umeme.

Biblia inasema Malaika alishuka toka mbinguni kwenye kaburi la Yesu ambapo wale walinzi walipomwona walizimia wakawa kama wafu, ndipo tunaanza kufahamu kwanini Malaika wawili peke yao waliichoma sodoma na gomora. Unapoomba saa nyingine haujibiwi sababu unaagiza Malaika elfu moja wakati Malaika mmoja anatosha kumpiga yule anayekusumbua.

MATHAYO 28: 1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.”

Malaika ni roho watumikao katika Ufalme, kila mtu aliye ndani ya Ufalme anao Malaika wake wa kumtumikia. Unapokuwa kwenye Ufalme unatakiwa uwatumie Malaika na sio kuwaabudu unasema katika jina la Yesu namtuma Malaika aende afanye kitu fulani.
NDANI YA UFALME MALAIKA WA KUFANIKISHA NJIA

MWANZO 24: 40 “akaniambia, bwana, ambaye naenenda machoni pake, atapeleka Malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu.”

Kuna Malaika wa kukuokoa na maovu.

MWANZO48: 16 “naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, ibrahimu na isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.”

KUNA MALAIKA WA KUKUTANGULIA NJIANI.

KUTOKA 23: 20 “tazama, mimi namtuma Malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.”

KUNA MALAIKA ANAYEKUPELEKA KWENYE HATIMA YAKO.
MALAIKA WA KUKUTOA SEHEMU MBAYA HASA UTUMWANI.
kuna utumwa wa muda mrefu anaweza kuwa nao na huyu ndiye aliyetumwa na Mungu kwenda kuwaokoa wana wa Israeli.
HESABU 20: 16 “tena tulipomlilia bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma Malaika, na kututoa tutoke misri; nasi tupo hapa kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho”

Kuna Malaika wa utia nguvu.

Kuna Malaika wa kuamsha moyo uliolegea, anakuamsha uanze upya pale unaporudi nyuma.

Kuna Malaika wa kufanya vituo kuwazungukia watakatifu wale wamchao Mungu.

Kuna Malaika wa Kulinda katika njia zao zote.
Kuna Malaika wa Kuwazungukia wamchao na kuwaokoa.

ZABURI 34: 7 “Malaika wa bwana hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.”

Kuna Malaika wa Kuwaangusha chini watesi.
ZABURI 35: 5 “wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa bwana akiwaangusha chini.”

Unapoomba unamtaja malaika huyu kukufanyia kazi ya kumwangusha chini yule mtu anayekutesa na kukusumbua. Anaweza kuangusha uchumi wake, nguvu zake, lile tegemeo lake analolitegemea ili aishi.

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA
ZABURI 78: 49 “akawapelekea ukali wa hasira yake, ghadhabu, na uchungu, na taabu, kundi la Malaika waletao mabaya.”

Kwenye Ufalme wa Mungu kwenye Biblia imeandikwa roho ya Mungu ikamwacha sauli na roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamuingia, kimsingi kuna Malaika waovu ambao wanaisikia sauti ya Mungu na Biblia inasema mtego alioutega umnase mwenyewe. Kwa jina la Yesu.

MALAIKA WAWE UPEPO

ZABURI 104: 4 “huwafanya Malaika zake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa moto wa miali.”

WAEBRANIA 1: 7 “na kwa habari za Malaika asema, afanyaye Malaika zake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa miali ya moto.”

MALAIKA WA KUINGIA NAO NDANI YA MATATIZO.

DANIEL 2: 28 “lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi”

Walikuwa watu watatu waliotakiwa kuingia kwenye moto pamoja lakini Mungu alimtuma Malaika wake akaingia nao ndani ya moto na akatoka nao, kwenye maisha unaweza ukawa una tatizo limekushika ama ugongwa ama ndugu yako anaumwa au kazini au kwenye biashara na unapomtuma Malaika huyu anakwenda anakaa na wewe kwenye tatizo na baadaye utakapotoka usiwe na harufu ya tatizo ulilokuwa nalo.

“Baba Kwa jina la Yesu naamuru malaika wa kuingia name kwenye shida iliyonipata aingie na mimi na nikitoka nisinukie shida yenyewe kwa jina la Yesu Amen. Unaweza kumwamuru malaika huyu akawa na wewe kwenye shida yeyote na Mungu akakusaidia mpaka ukatoka kwenye shida hyo.

KUNA MALAIKA WA KUFUNGA MAKANO YA SIMBA.

Malaika huyu ni Malaika ambaye anashughulika na midomo. Unaweza kumtuma Malaika huyu akaenda kuwafunga midomo wale watu wananaokuongelea mambo yasiyofaa na wakaacha mara moja kwa jina la Yesu

DANIEL 6: 22 “Mungu wangu amemtuma Malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, ee mfalme, sikukosa neno.”

KILA KANISA KWENYE AGANO JIPYA KULIKUWA NA MALAIKA MAALUM WA KULINDA KANISA.

UFUNUO 2: 1 “kwa Malaika wa kanisa lililoko efeso andika; haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.” 8 na kwa Malaika wa kanisa lililoko smirna andika; haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. 12 na kwa Malaika wa kanisa lililoko pergamo andika; haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 7 na kwa Malaika wa kanisa lililoko filadelfia andika; haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.”

KUNA SHERIA YA MALAIKA WA MAJI

UFUNUO 16: 5 “nami nikamsikia Malaika wa maji akisema, wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi”

Kwenye maombi yako unaweza kumtumia Malaika huyu wa maji akaenda kwa yule mchawi anayelima kwa uchawi mvua ikanyesha shambani mwake na kuharibu kila kitu. “Sisi tunazo nguvu kuliko wachawi na waganga wa kienyeji”

MALAIKA ANAYESHUGHULIKIA UPEPO.

Unaweza kumtuma akasimamisha upepo kwa wale wanaoharibu mambo yako kutokea baharini, nchi kavu au angani ukamwagiza akaenda kuharibu mipango yao kwa jina la Yesu, tunatakiwa tuishi kwenye imanikama ya eliya ya kuamuru mvua simama usinyeshe miaka mitatu na isinyeshe.

Ukiri
Baba wa mbinguni katika jina la Yesu ninaamuru malaika wa kutuliza upepo nenda katulize upepo wa kuyumba kiuchumi kwenye familia yangu kwa jina la Yesu, naamuru tuliza matatizo yote yanayotumwa na wachawi na wasoma nyota na waganga wa kienyeji kuja kwangu kwa jina la Yesu……Amen”

NA :  ASKOFU  MKUU Dr  JOSEPHAT  GWAJIMA

UFUFUO NA UZIMA